BREAKING NEWS:Abiria wahofiwa kupoteza maisha ajali ya daladala


Watu kadhaa wanaripotiwa kupoteza maisha katika ajali iliyotokea muda huu jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo inahusisha Daladala kutoka Temeke kwenda Muhimbili kwa kugongana na Lori la mchanga.

Katika ajali hiyo iliyotokea Mataa ya Chang’ombe wilayani Temeke jijini humo pia imesababisha majeruhi kwa watu kadhaa. Mwandishi Diramakini atakujuza punde kinachojiri...

Update Live

DAR ES SALAAM 05.10.2020

Mpaka sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea majeruhi watano kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke waliopata ajali leo asubuhi  05.10.2020 eneo la Chang'ombe-Temeke.
1. William Paul Akida (Me-42)
2. Jina halijafahamika (Me-32)
3. Jina halijafahamika (Me-20)
4. Alicia Teophil (Ke-25)
5. Valentino Lucas (Ke-29)
Wanaendelea na matibabu. Haya yamethibithishwa na Aminiel Aligaesha 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano 
Hospitali ya Taifa Muhimbili.

DAR ES SALAAM 05.10.2020

Katika ajali hiyo watu watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa vibaya.
 
Amon Kakwale ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Makamanda hao wamesema kuwa, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi zaidi, Mwandishi Diramakini anaendelea kukujuza hatua kwa hatua, endelea kufuatilia hapa ...
Muonekano wa daladala iliyogongana na Lori leo mapema Oktoba 5,2020 katika Mataa ya Chang'ombe wilayani Temeke,Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa daladala.
#DiramakiniJaliuhaiAchamwendokasi
 Kwa upande wake Mkuu wa Wiaya ya Temeke, Godwin Gondwe amesema mpaka sasa dereva hajulikani alipo, kwani mara baada ya ajali hiyo alitoweka na kukimbilia
 kusikojulikana.

"Niwape pole familia ambazo wamepoteza wapendwa wao, ambapo mpaka sasa hivi wamefariki 5 na majeruhi 10, inaonekana ni uzembe wa madereva maana wakati wanatoka Buza abiria walikuwa wanamuambia apunguze mwendo na alipofika kwenye mataa, taa nyekundu ilikua imewaka, abiria wakmkumbusha lakini akawaambiwa wasimfundishe kazi dereva yeye kakimbia na lakini serikali ina mkono mrefu tutamfikia, nitoe wito kwa madereva wa dalaladala wamebeba uhai wa watu, mali zinatafutwa, uhai wa mtu ukipotea hauwezi kurejea kwa hiyo wafuate sheria ili kuokoa maisha,"amesema

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news