DKT. BASHIRU AONGOZA MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS DKT.MAGUFULI ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameongoza mapokezi ya kumpokea mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mapokezi hayo, yamefanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar leo tarehe 02 Oktoba, 2020 ambapo Mhe. Dkt. Magufuli ameeleza kwa ufupi, 

"Leo nimeingia hapa Zanzibar, nimeingia Zanzibar kwa ajili ya kuja kufanya Kampeni, kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi."

Mgombea wa Urais wa  CCM Mhe. Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni kesho tarehe 03 Oktoba, 2020 katika viwanja vya Mnazi  mmoja Mkoa wa Mjini.

Imetolewa na;

Said Said Nguya

Afisa Habari

Ofisi ya Katibu Mkuu

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news