Dodoma Jiji FC yaipeleka Tanzania Prisons FC uwanja wa Samora

Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji FC umesema kuwa, mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara mzunguko wa nane dhidi ya Tanzania Prisons FC utachezwa kwenye Uwanja wa Samora uliopo Manispaa ya Iringa Oktoba 26,2020 (Jumatatu), badala ya Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kama ilivyopangwa awali, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC, Ramadhani H.Juma mabadiliko hayo yanafuatia Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuwa na matumizi mengine ya tarehe ya mchezo. "Mchezo utachezwa saa 10:00 jioni na kiingilio ni shilingi elfu tatu (3,000) tu," amefafanua Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC, Ramadhani H.Juma.

Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar FC mkoani Kagera, timu ya Dodoma Jiji FC imerejea na kuanza programu ya gym ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Oktaba 26,2020 katika Uwanja wa Samora uliopo mkoani Iringa.

No comments

Powered by Blogger.