Hatua kwa hatua utekelezaji Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115)

"Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) kwenye bonde la mto Rufiji unaendelea kwa kasi inayohitajika;...

Utekelezaji wa mradi umetokana na Sera ya Nishati ya Mwaka 2015. Sera hiyo ina lengo la kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hata hivyo, kwa kuzingatia kasi na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano, lengo la awali la kisera limeongezewa nguvu zaidi kwa kuwekewa ukomo mpya kwamba sasa wananchi wote wawe wameunganishwa na huduma ya umeme kufikia mwaka 2022 ikiwa ni kabla ya lengo/ukomo mkuu wa mwaka 2025. 

Mradi huu unatajwa kuwa ni ufunguo wa kufikia malengo hayo.Aidha, Mpango Kabambe wa Sekta ya umeme umetoa maelekezo ya kimkakati ya kuendelea kubuniwa vyanzo zaidi vya uzalishaji 
umeme. 

Utekelezaji wa Mradi huu utasaidia kufikia mikakati hii, lakini pia kuisaidia nchi kutimiza wajibu wake wa kidunia kupitia Malengo ya Mendeleo Endelevu (SDGs) hasa malengo mahsusi yafuatayo:

Lengo 1. Kuondoa umaskini
Lengo 7: Upatikanaji wa nishati rahisi na 
salama kwa mazingira; na 
Lengo 9: Kuendeleza Viwanda, Ubunifu na 
Miundombinu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news