Kurasa za magazeti ya Kiswahili Oktoba 17,2020 'ogoba matapeli,Dube hauzwi'
Gazeti mahususi kwa michezo la Bingwa linaripoti kuwa, "ogoba matapeli,Dube hauzwi". Mwandishi Diramakini amebainisha kuwa, Dube anayetajwa hapa ni yule mshambuliaji wa timu ya Azam FC ya Dar es Salaam, Prince Dube ambaye alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2020/21.

Dube alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali, ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Kwa mwezi huo wa Septemba ambao ulikuwa wa kufungua msimu, kila timu ilicheza michezo minne na Dube alionesha kiwango kikubwa na kuiwezesha Azam kushinda michezo yote, hivyo kupata pointi 12 na kuongoza ligi ambapo Dube alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja iliyozaa bao. Azam ilizifunga Polisi Tanzania FC 1-0, Coastal Union FC 2-0, Mbeya City FC 0-1 na Tanzania Prisons FC 0-1.

Dube aliwashinda kipa wa Azam, David Kissu na kiungo wa Simba SC, Clatous Chama ambapo Kissu aliiongoza Azam kushinda katika michezo yote bila ya kuruhusu bao, hivyo timu hiyo kuongoza ligi na hadi sasa inaendelea kuongoza wakati Chama aliiongoza Simba kushinda michezo mitatu na kutoka sare mmoja, huku akifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za usaidizi wa bao na achezaji wote hao hawakupata kadi yoyote.


No comments

Powered by Blogger.