Maalim Seif:Membe unatuchanganya, Membe asisitiza ni yeye

Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa leo Oktoba 20,2020 ametoa msimamo wa chama hicho kuhusu mgombea urais wa chama hicho, Bernard Membe huku akimtaka asiwachanganye wanachama wa chama hicho kwani msimamo wao upo pale pale.

Kwa hiyo tulikubaliana kwamba kama vyama makini havitashirikiana itakuwa vigumu kuiondoa CCM, hivyo ulitoa mamlaka kwa vikao vingine vya chama kuhakikisha ACT inafanya kila juhudi kushirikiana na vyama makini kwenye uchaguzi wa mwaka huu

Ametoa msimamo huo ikiwa ni siku moja baada ya ndugu Membe kuzungumza na waandishi wa habari na kutangaza msimamo wake kwamba yeye bado ni mgombea halali wa chama hicho na anaendelea na kampeni kuelekea Oktoba 28,2020.

Maalim Seif amesema anasikitika kwa kauli iliyotolewa na Membe jana kwani ACT-Wazalenzo kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, walikubaliana kwamba yanahitajika mabadiliko.

Pia Maalim Seif amesema, kwa sasa hakuna taarifa yoyote kwamba kuna mwanachama anapinga msimamo wa chama hicho kushirikiana na CHADEMA, hivyo wataendelea kumuunga mkono Tundu Lissu katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amehoji, Je? (Bernard Membe) umeletwa ACT Wazalendo kwa lengo maalum, sisi tupo macho na upinzani mara hii ni imara na upo tayari kuiondoa CCM, kwa hiyo hata msimamo wa chama hatujasema tunawaunga mkono wagombea wote wa CHADEMA na wala wao hawajasema wanaunga mkono wagombea wote wa CHADEMA, hiyo ipo kwenye vichwa na yapo baadhi ya majimbo wamekubaliana wao wenyewe kuachiana majimbo,"amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amesema, Bernard Membe alipojiunga na ACT Wazalendo walimwambia kwamba maazimio ya Mkutano Mkuu ni kushirikiana na vyama vingine makini vya upinzani na kwamba yeye alikubaliana na hilo, lakini leo hii inashangaza kusikia anasema anaendelea na kampeni jambo ambalo halipo.

Maalim Seif amesema amehoji kuwa, je? Hizo kampeni zake mmeziona? Baada ya kuona kampeni zinakwenda takribani mwezi mmoja na nusu za kwake zimesuasua tulikutana katika Kamati ya Uongozi na kushauriana na Membe akiwepo.Tulishauriana kwamba mgombea wetu haonekani, afadhali ya mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana. Membe alisema ikifika tarehe fulani hajaanza kampeni waanze kumuunga mkono Lissu. Mimi kama Mwenyekiti wa chama moja ya majukumu yangu ni kusimamia maamuzi ya chama, kwa hiyo maamuzi yaliyotolewa na vikao hivyo ni jukumu langu kuyasimamia.

Wakati hayo yakijiri, Mgombea Urais wa Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe amesema yeye ndiye amethibitishwa katika nafasi ya kuwania urais na anaendelea na kampeni.

No comments

Powered by Blogger.