Mwalimu ajinyonga baada ya watoto kupata Corona

Mwalimu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 47 katika Manispaa ya Dulag iliyopo Jimbo la Leyte jijini Tacloban, Ufilipino amejinyonga baada ya kubaini kuwa, watoto wake wawili wameambukizwa virusi vya Corona (COVID-19), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa Gazeti la kila siku la Tempo nchini humo, jeshi la polisi limethibithisha kutokea kwa tukio hilo la mwalimu ambaye alikuwa anafundisha shule ya umma.

Mwalimu huyo inaelezwa amejinyonga jana majira ya saa sita mchana ambapo mwili wake ulikutwa ukining'inia juu. Kwa mujibu wa mume wa mwalimu huyo ambaye pia ni mwalimu katika moja ya shule za umma jijini humo, mkewe alikabiliwa na msongo mkali wa mawazo baada ya watoto wake hao wawili kupimwa na matokeo kuthibithisha wana maambukizi ya corona.

"Mke wangu hakuweza kulala kwa siku mbili na sikufanikiwa kuzungumza naye japo kidogo usiku kabla ya tukio hili na sikutarajia haya kutokea," amenukuliwaEndelea hapa.

No comments

Powered by Blogger.