Mwalimu Makuru: Mgombea anasema sisi ni ombaomba, akimaliza kujinadi naye anatembeza bakuli, msifanye makosa

Watanzania wameaswa kuzipuuza kauli za baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wanaoomba kura kwa kubeza mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na madai yao wanayosema kwamba Tanzania ni maskini, anaripoti Amos Lufungulo (Diramakini), Mara.

Wamehimizwa, kuyaona kwa mtazamo chanya maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mitano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli na hivyo basi, wapuuze madai ya kauli zinazosemwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kwamba Tanzania haijaendendelea wala kuwa na mabadiliko yoyote kwa miaka mitano, kwani kila mmoja anayaona yaliyotendeka kwa macho.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakifuatilia kampeni za Mgombea Udiwani Kata ya Kitaji Wilaya ya Musoma Mjini mkoani mara, Icon Emmanuel Nestory. (DIRAMAKINI)

Hayo yamesemwa na Mwalimu Makuru Lameck Joseph aliyekuwa miongoni mwa makada wa CCM waliojitosa kuomba kuteuliwa na chama hicho kwenye kura za maoni kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini wakati akiomba kura za mafiga matatu katika Kata ya Kitaji Manispaa ya Musoma, ambapo amesema Watanzania watembee kifua mbele na kujivunia kazi nzuri za kimaendeleo zilizofanywa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

"Kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akisema Watanzania ni matajiri lazima tukubaliane na kauli hiyo, tumeona miradi mingi ya kijamii na kiuchumi ikiwemo reli ya kisasa, ndege na mingine mingi ikigharimiwa kwa fedha zetu za ndani, lakini pia rasilimali zetu amezilinda kwa dhati mfano bora mikataba ya madini kuiboresha itunufaishe Watanzania na sekta ya utalii ambayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu. Hao wanaosema nchi ni masikini na ni ombaomba wapuuzwe imefikaje uchumi wa kati pasipo kazi nzuri ya Awamu ya Tano,"amesema Mwalimu Makuru.

Mwalimu Makuru Lameck Joseph akihutubia katika mkutano huo. (DIRAMAKINI).

"Niwaombe Watanzania wote tukafanye uamzi wa maisha yetu kwa miaka mingine mitano Oktoba 28 mwaka huu, tumpigie kura kwa wingi za ushindi Rais Magufuli, Mbunge Mathayo na Mgombea wa kata yetu ya Kitaji Icon Emmanuel Nestory, tusidanganyike kuchagua wagombea wa vyama ambavyo hawawezi hata kidogo kututatulia kero zetu na kutuletea maendeleo ambayo yatatutoa hapa tulipo na kutupeleka mbali zaidi,"amesema Mwalimu Makuru.

Aidha, Mwalimu Makuru amesikitishwa na baadhi ya wagombea wa Urais wanaobeza Watanzania na kusema kuwa ni ombaomba, wakati huo huo baada ya mikutano yao kumalizika hupitisha bakuli na kuomba kuchangiwa fedha kwa ajili ya kampeni zao jambo ambalo ni ishara ya kuwadhihaki watanzania.

"Mtu anasema nchi ni ombaomba na baada ya mkutano wake kumalizika anaomba mchango, naomba Watanzania tuwe makini sana na viongozi wa namna hii tukiwapa nafasi wanaweza kutekekeza Taifa maana kwa kauli zao tu haziaminiki, sembuse tukiwapa nafasi za kutuongoza,"amehoji.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa Kata ya Kitaji, Icon Emmanuel amesema endapo watamchagua Oktoba 28, mwaka huu kuwa diwani wa kata hiyo, atawawakilisha vyema kwa kuweka mazingira bora ya wafanyabiashara, kushughulikia mikopo kwa wepesi.

Sambamba na kuwaunganisha kwa pamoja wananchi wa kata hiyo katika kuhakikisha kwamba, Kitaji inakuwa na maendeleo ya uhakika katika nyanja ya kiuchumi na kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news