Rais Trump, mke wake Melania wathibitika kuwa na Corona

Rais wa Marekani, Donald Trump na mke wake Melania Trump wamethibitka kuwa wameambukizwa virusi vya Corona (Covid-19), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Matokeo hayo yanakuja siku moja baada ya mshauri wake wa karibu kuthibitika ana COVID-19 baada ya kusafiri naye kupitia ndege ya Air Force One.

"Hope Hicks, ambaye amekuwa akitimiza majukumu yake bila kuchoka na bila kupumzika hata kidogo, amegundulika ana maambukizi ya Covid-19.Ni tatizo, Mke wangu na Mimi tunasubiria matokeo ya vipimo, hivyo muda wowote tutaanza mchakato wa kukaa karantini,"amesema awali Rais Trump kupitia ukuta wake wa Twitter kabla ya matokeo ya sasa ambayo yamethibitisha rasmi Covid-19.

Post a Comment

0 Comments