Serikali yakutana na wazalishaji wa saruji nchini

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji,Angellah Kairuki wamefanya kikao cha pamoja na wazalishaji wa saruji nchini kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali, changamoto na namna bora ya kukuza sekta ya ujenzi nchini kupitia saruji, kikao kilichofanyika Ofisi za Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), jijini Dar es Salaam,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wakurugenzi wa kampuni tisa za saruji zikiwemo Dangote Cement, Camel Cement, Nyati Cement, Mbeya Cement, Kilimanjaro Cement, Maweni Cement, Tanga Cement, Lake Cement, Twiga Cement pamoja na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) wakiwa katika kikao cha pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji,Angellah Kairuki wakijadili masuala mbalimbali na wazalishaji wa saruji nchini kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na namna bora ya kukuza sekta ya ujenzi nchini kupitia saruji, kikao kilichofanyika Ofisi za Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17,2020. (WVB).
Katika kikao hicho cha leo Oktoba 17,2020, mawaziri hao wamekutana na kampuni tisa za saruji zikiwemo Dangote Cement, Camel Cement, Nyati Cement, Mbeya Cement, Kilimanjaro Cement, Maweni Cement, Tanga Cement, Lake Cement, Twiga Cement pamoja na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) na kujadili namna bora ya kuendeleza sekta hiyo.

Waziri Bashungwa amewapongeza wazalishaji hao kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwasihi wasipandishe bei ya saruji kiholela hasa kuzingatia kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya 5 ni kuiona Tanzania inakua nchi ya viwanda.

Wazalishaji hao wamezungumzia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo ubovu wa barabara hasa kipindi cha mvua, unaofanya bei kuwa juu kidogo, upatikanaji wa nishati madhubuti kama gesi, suala la kodi na kuiomba serikali sikivu kushughulikia changamoto hizo.

Nae Waziri Kairuki amesema kuwa wizara yake na Wizara ya Viwanda wanafanya kazi kwa ukaribu na kuwatoa hofu wazalishaji hao wa saruji kuwa serikali ipo pamoja nao na inashughulikia changamoto zao na kuwahakikishia wizara yake yenye dhamana ya uwekezaji itahakikisha inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hao.

Aidha,Waziri wa Viwanda na Biashara,Innocent Bashungwa amewahakikishia wazalishaji hao kuwa serikali ina angalia namna bora ya kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi hasa kwa viwanda vilivyopo Ukanda wa Pwani pia amewahakikishia kuwa changamoto nyingine ndogo ndogo atazishughulikia ndani ya wiki moja ijayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news