TAKUKURU yaonya Uchaguzi Mkuu, yafuatilia miradi Lindi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imeonya vitendo vya rushwa katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu huku ikibainisha kuwa, makachero wake wanaendelea kufuatilia miradi ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 22, mwaka 2020 na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi, Charles Mulebya.

"Mkoa wa Lindi unajumuisha wilaya tano ambazo ni Lindi, Kilwa, Nashingwe,Liwale na Ruangwa. Katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 ilioanzia mwezi Julai,2020 hadi Septemba, 2020. Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Lindi imefanya kazi na kutekeleza majukumu mbalimbali kwa na,mna yanavyoainisha katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2019. Majukumu hayo yalifanywa kupitia madawati mbalimbali ikiwemo dawati la uchunguzi, huduma za sheria na mashitaka. Utafiti na udhibiti na elimu kwa umma.

"Kupitia dawati la uchaguzi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2020,TAKUKURU Mkoa wa Lindi ilipokea jumla ya malalamiko haya yanafanyiwa kazi na yapo katika hatua mbalimbali na baadhi yamekamilika. Pia kesi mpya mbili zimefunguliwa,"amesema.

Wakati huo huo, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi, Charles Mulebya amesema kuwa, taasisi hiyo mkoani hapa imeokoa kiasi cha shilingi 327,119,853.00.

Fedha hizo zilizookolewa zinajumuisha fedha za wakulima kwa mauzo ya ufuta na korosho, miradi mbaimbali ya maendeleo na kodi ya mapato ya Serikali. "Kati ya fedha hizo shilingi 145,143,020 zilirejeshwa serikalini na shilingi 181,976,833 zilikabidhiwa na kurejeshwa kwa wahanga. Kwa upande wa mashitaka, katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2020 TAKUKURU Mkoa wa Lindi ilifanikiwa kufungua jumla ya kusi mpya mbili.

Mbalimbali na wadau wengine juu ya rushwa n a madhara yake kwa mtu mmoja mmoja, jamii, taasisi na taifa kwa ujuma. Amesema, TAKUKURU Mkoa wa Lindi imeendesha semina 23, imefanya mikutano yas hadhara 40. Pia TAKUKURU Mkoa wa Lindi imefanya ufunguzi na uimarishaji wa klabu za wanafunzi za wapinga rushwa 28,vipindi vya TV na redio vinne.

Naibu Mkuu huyo amesema, katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na majukumu mengine TAKUKURU Mkoa wa Lindi imejipanga kuongeza juhudi katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati iliyopo mkoani Lindi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara na maji, kuchambua mifumo ya ukusanyaji wa kodi na mapato ya Serikali, na kuendelea kuelimisha umma madhara ya rushwa katika uchaguzi hususani Uchaguzi Mkuu na madiwani,wabunge, na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.

"Pia, TAKUKURU Mkoa wa Lindi inaendelea kutoa wito kwa wananchi, wagombea, mawakala wa wagombea katika nafasi mbalimbali, vyama vya siasa na wadau wote katika Mkoa wa Lindi kuwa wanapaswa kuzingatia sheria , kanuni na taratibu kujiepusha na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huu mkuu, kinyume na hapo hatua stahiki zitachukuiwa kwa wote watakaobainika kutenda makosa,"amesema.

"TAKUKURU Mkoa wa Lindi inaendelea kuwashukuru na kuzishukuru taasisi mbalimbali (binafsi na za Serikali) Mkoa wa Lindi kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa ofisi yetu na zaidi TAKUKURU.

"Aidha, tunawaomba waendelee kutuunga mkono kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa kutumia njia mbalimbali hususani kupitia simu yetu ya 133, kwani mapambano dhidi ya rushwa sio ya TAKUKURU peke yake bali ni jamii nzima kwa ujumla," ameeleza Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi, Charles Mulebya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news