TAKUKURU yawezesha wafanyakazi mashamba ya Thomas Meliyo Rikoyan kulipwa madai yao

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara imewezesha kupatikana na hatimaye kulipwa wafanyakazi vibarua 27 jumla ya shilingi milioni 17,737,887 walizokuwa wanamdai, Bw. Thomas Meliyo Rikoyan mkulima mkubwa wilayani Simanjiro, anaripoti Mwandishi Diramakini. 

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara, Adam Kilongozi ameyabainisha hayo leo Oktoba 19, 2020.

Bw. Thomas Meliyo Rikoyan mwenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu mbili wilayani Simanjiro ameajiri kwa kuwaweka kambini kwake vibarua 27, kazi yao ikiwa ni kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna, kupukuchua (mahidi) na kupigapiga maharage.

"Mnamo Oktoba 9, 2020 TAKUKURU Mkoa wa Manyara ilipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya vibarua hao wakimlalamikia Bw.Thomas Meliyo Rikoyan kwamba tangu mwezi Novemba,2019 hadi sasa wamekuwa wakifaya kazi kwenye masdhamba yake bila kulipwa mshahara kinyume na makubaliano ya mikataba ya ajira zao.


"Shilingi  milioni 26,000,000 ziliokolewa na kurejeshwa halmashauri kutoka kwa Bw.Mourice Dastan Bendera wa KOIYA General Supply. (Ni rai yetu kwa kamati za tathmini katika taasisi nunuzi kufanya kazi zao kwa uadilifu ili kupata wazabuni wenye uwezo, kushindwa kufanya hivyo kutatulazimisha kuanza uchunguzi dhidi ya kamati hizo," amefafanua Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara, Adam Kilongozi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news