Tetesi:Ismaila Sarr, Troy Deeney wajitolea kuirudisha Watford ligi kuu

Kwa mujibu wa The Independent beki wa kulia wa Ureno, Ricardo Pereira (27) ambaye alifanyiwa upasuaji wa jeraha la goti anatarajia kurejea ndani ya wiki sita zijazo kuichezea Klabu ya Leicester City.

Huku London Standard ikiripoti kuwa, bosi wa Watford, Scott Duxbury amesema winga wa Senegal, Ismaila Sarr (22) na mshambuliaji Troy Deeney (32) wamejitolea kuisaidia klabu hiyo kurudi Ligi Kuu.

Wakati kwa upande wa Express ni kwamba beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini meneja Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo yao juu ya uhamisho kwenye dirisha la msimu wa joto.

Daily Record inaripoti kuwa, kiungo wa zamani wa Celtic na Rangers, Liam Burt (21) alikuwa huko Pittodrie kwa pambano la Aberdeen la Premiership na Hamilton huku akienaendelea kutafuta nafasi kwenye vilabu vingine.

Kwa upande wa Mail inaripoti kuwa, mlinzi wa zamani wa Arsenal, Per Mertesacker anasema kiungo wa kati wa Ujerumani, Mesut Ozil mawazo yake yapo mbali na mpira wa miguu.Mchezaji huyo wa miaka 32 ameachwa kwenye kikosi cha Arsenal katika Ligi Kuu ya siku ya Jumanne.

Mbali na hayo, The Athletic inaripoti kuwa, Klabu ya Tottenham wapo mbioni kuingia mkataba mpya wa muda mrefu na mshambuliaji wa Korea Kusini, Son Heung-min (28).

No comments

Powered by Blogger.