Tetesi:Kylian Mbappe anaweza kutua Liverpool, Real Madrid

Kwa mujibu wa Le Parisien, mshambuliaji Kylian Mbappe (21) anaweza kuondoka Paris St-Germain kuelekea Liverpool au Real Madrid msimu ujao. Huku Football Insider, Klabu ya Tottenham ina mpango wa kufanya mazungumzo na Danny Rose (30) kuhusu suala la kusitisha mkataba wake mapema.
Nayo Klabu ya Brighton inaelekea kukubali Euro milioni 50 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati Ben White kama Liverpool itahitaji mchezaji atakayechukua nafasi ya mchezaji wa Uholanzi, Virgil van Dijk (29) hii ikiwa ni kwa mujibu wa Sun.

Mail inaripoti kuwa, winga wa England, Mason Greenwood (19) amezungumza na Manchester United kuhusiana na suala la kuzingatia muda ambapo Sun inadokeza kuwa, mshambuliaji wa England, Danny Welbeck (29) amekataa ofa ya Euro 140,000 kwa wiki kutoka kwenye Ligi ya Uturuki ya Super League  Club akiamini kuwa Fenerbahce itabaki kwenye Ligi ya Premia ikiwa na Brighton.

Aidha, Meneja wa Aston Villa Dean Smith amesema, mkataba wa kudumu wa mchezaji wa mkopo wa Chelsea, Ross Barkley (26) bado haujajadiliwa hii ikiwa ni kwa mujibu wa Birmingham Mail.

Wakati huo huo, Sun inaripoti kuwa, kiungo wa kati wa Ureno, Gedson Fernandes (21) ambaye yupo kwa mkopo Tottenham kutoka Benfica, anaonekana atarejea haraka katika klabu yake ya nyumbani mwezi Januari,mwakani baada ya kushindwa kuwavutia Lilywhites.

No comments

Powered by Blogger.