Tetesi:Paul Pogba anataka kandarasi na Barcelona

Kwa mujibu wa Mail,Manchester United haikuwasilisha ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa, Kingsley Coman (24) ni wakati wa dirisha la usajili.

Hayo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo ya Ujerumani ya Bayern Munich,Hasan Salihamidzic. Wakati huo huo, Sky sports inaripoti kusa, Klabu ya
West Brom imekubaliana na ada ya uhamisho ya karibu £15milioni na klabu ya Huddersfield kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji Karlan Grant (23). 
Paul Pogba. (Getty Images).

Mundo Deportivo inaripoti kuwa,kiungo wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba, (27) anataka kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru dirisha lilajo la usajili la majira ya joto. Huku Manchester Evening ikiripoti kuwa, Klabu ya Juventus imeungana na Manchester City katika mbio za kumuania mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba (28). 

Wales Online inaripoti kuwa,Liverpool wako tayari kumuachia kwa mkopo Harry Wilson (23), lakini ilikataa ofa ya Swansea City kwa ajili ya winga huyo.

Athletic imeweka wazi kuwa, mlinzi wa Ujerumani, Antonio Rudiger (27) amesema, anataka kurejesha nafasi yake ndani ya kikosi cha Chelsea baada ya uhamisho wake kukwama katika dirisha la usajili lililopita huku Sports Illustrated ikiripoti kuwa,mshambuliaji wa Manchester City na Argentina,Sergio Aguero (32) hana mpango wa kuhamia Italia licha ya kusakwa na klabu ya Inter Milan ya ligi ya Serie A. 

Express imebaini kusa, Klabu ya Chelsea wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wake kutoka Italia, Jorginho ambaye alihusishwa na mipango ya kuhamia Arsenal wakati wa dirisha la usajili lililopita huku Meneja wa zamani wa Juventus, Max Allegri anaweza kuwania nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer , kama Manchester United itamtimua kocha wake huyo. 

No comments

Powered by Blogger.