Utafiti:Dkt.Magufuli atamshinda Lissu

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli ataibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,mwaka huu,anaripoti Rachel Balama (Diramakini) Dar es Salaam.

Hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa maoni ya Watanzania kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020 uliofanywa na Kampuni ya Teknolojia na Utafiti ya Gharus. 

Akitoa matokeo ya utafiti huo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kitengo cha Mahusiano, Elena Ryafanova amesema, utafiti huo umefanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia mwezi Juni hadi Oktoba, mwaka huu. 

Amesema, maoni yamekusanywa kutoka kwa watu 48,239 wenye umri zaidi ya miaka 18 wa jinsia zote na kwamba asilimia 58 ya washiriki wa utafiti huo ni wanawake na asilimia 42 ni wanaume. 

Maoni ya utafiti kulingana na maeneo ya kupigia kura katika baadhi ya mikoa na asilimia atakazopata mgombea huyo wa CCM, Pamba 55, Unguja 84, Simiyu 90, Moshi 68, Mwanza 77, Dodoma 86, Arusha 67 na Dar es Salaam 72.

Kwa mujibu wa utafiti huo kwa mgombea Tundu Lissu ni kama ifuatavyo katika mikoa na asilimia Pemba 43,Unguja 14, Simiyu 8, Moshi 30, Mwanza 20, Dodoma 12,Dar es salaam 27 na Arusha 31 huku wagombea kutoka katika vyama vingine wakiambulia asilimia kati ya moja na mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news