Wanafunzi wakiri mbele ya polisi kujihusisha na wizi vifaa vya shule

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi watatu kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa vya ujenzi wa shule, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa 12 jioni ya Oktoba 15, mwaka huu katika Kijiji cha Manoleo Kata ya Itonjanda  iliyopo Manispaa ya Tabora.

Amesema, wanafunzi hao ni wa Shule ya Sekondari Itonjanda ambao wanakabiliwa na tuhuma za kuiba mifuko minne ya saruji,viti vitano na nondo tano zote mali ya Shule ya Msingi Manoleo ambapo baada ya kubanwa wamekiri kutenda hivyo na hatua zaidi zitachukuliwa.

Kamanda amesema kuwa, majira hayo walimkamata Hasani haruna (18) mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Itonjanda na wenzake wawili ambao ni wanafunzi wakiwa na vitu hivyo.

No comments

Powered by Blogger.