Waziri Mkuu Jacinda Ardern apata ushindi mkubwa

Leo Oktoba 17,2020 Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri Mkuu Jacinda Ardern. (Reuters).
Ushindi huo wa kishindo leo unakifanya chama chake cha Labour kuwa na nafasi ya kuunda serikali bila ya kuvishirikisha vyama vingine nchini humo,hivyo kumuwezesha kutekeleza mpango wake wa mageuzi.

Baada ya kuhesabiwa theluthi mbili ya kura zote, chama cha Waziri Mkuu Adern cha Labour kimepata asilimia 49.2 ya kura zote, huku kikitarajiwa kupata viti 64 katika bunge la New Zealand lenye viti 120.

Chama cha upinzani cha mrengo wa kati wa kulia cha National Party kimeshinda asilimia 26.8 ambayo ni sawa na viti 35 katika uchaguzi huo ambao ulipaswa kufanyika Septemba, mwaka huu lakini ulisitishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19).
Aidha, hakuna kiongozi mwingine aliyeweza kupata ushindi mkubwa kiasi hicho tangu New Zealand ilipoidhinisha mfumo wa uchaguzi unaozingatia uwiano wa uwakilishi wa kivyama mwaka 1996.

No comments

Powered by Blogger.