Waziri Mkuu mstaafu Malecela amvaa Sheikh Ponda, ataka Watanzania wampuuze

Mapema leo Oktobata 20,2020 Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Malecela akiwa nyumbani kwake jijini Dodoma amejitokeza kuuasa umma wa Watanzania kutokana na kauli zilizotolewa na Sheikh Issa Ponda jijini Dodoma mwishoni mwa wiki katika majukwaa ya kisiasa wakati wa kumnadi Mgombea wa Urais wa Chama cha Chadema, Tundu Lisu, anaripoti Mwandishi Diramakini. 

Moja ya kauli za Sheikh Ponda katika kipidi hiki cha kampeni ni kuwa waumini wa dini ya Kiislam wamekubaliana nchi nzima kumchagua mgombea wa CHADEMA ili hali kauli hiyo inaonyesha uchochezi wa kidini nchini na badala yake amewataka kuhubiri amani, utulivu na usalama hasa kipidi hiki cha kampeni za urais, ubunge na udiwani.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Sheikh Ponda amesema, nchi hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ameiacha katika misingi ya umoja na amani, licha ya kuchukia uchochezi na ubaguzi kwa misingi ya udini na ukabila.

Mzee Malecela ametumia fursa hii kukemea na kuonya juu ya kuendekeza hali hiyo, jambo ambalo litapelekea mpasuko katika makundi ya jamii na wakati mwingine kupelekea machafuko.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Malecela ametoa rai kwa wananchi wa Tanzania kupuuza kauli hiyo kwa kuwa hakuna watu wanaoweza kuwalazimisha kumchagua mgombea kwa msingi wa dini yake bali waangalie vigezo ambavyo wanavipenda ikiwemo maendeleo na umoja wa Kitaifa na kuacha kuendelea kujadili vitu visivyokuwa na manufaa nchini na mwisho amewataka wanachi wote wa Tanzania kuwa watulivu katika wakati huu ambapo mchakato wa uchaguzi unachukua nafasi yake.
Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samuel Malecela.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news