Waziri wa Afya Kenya atoa angalizo dhidi ya Corona

Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe amesema huenda nchi hiyo ikakumbwa na maafa makubwa zaidi kutokana na wananchi hususani vijana kupuuza kanuni za kiafya dhidi ya virusi vya corona.

Oktoba 18, 2020 jijini Nairobi, Waziri Kagwe amesema kuwa, hali ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini humo si njema kwani, kwa jana kulikuwa na visa vipya 685.

Pia Waziri huyo amewakosoa wanasiasa ambao wanahutubia mikutano ya hadhara ambayo washiriki hawazingatii kanuni za afya za kuzuia corona kama vile kuvaa barakoa na kutokaribiana nchini humo.

Waziri Kabwe amesema, bado kuna wasiwasi mkubwa kutokana na kile alichoeleza ni wengi kujisahau huku wengine wakirejea katika majukumu yao ya kawaida, kwani kwa sasa kiwango cha maambukizo kimepanda kutoka asilimia nne hadi 12 baada ya Serikali kupunguza zuio karibuni.
Waziri wa Afya wa Kenya,Mutahi Kagwe.( The Star).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news