Chanjo ya Corona kuanza mwezi huu

Juhudi za wanasayansi zimeanza kuonyesha mwanga katika mafanikio ya chanjo ya kukabiliana na virusi vya Corona (COVID-19) ambapo kampuni ya kutengeneza dawa ya Moderna imesema inataka idhini ya dharura kwa ajili ya kutumia chanjo yake dhidi ya virusi hivyo, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, kwa sasa wanahitaji ridhaa hiyo ili waweze kuanza kuisambaza katika mataifa mbalimbali ikiwemo barani Ulaya na Marekani.

Wachambuzi wa masuala ya afya wameidokeza Diramakini blog kuwa, huenda chanjo hiyo ikwa na mafanikio kutokana na namna ambavyo kampuni hiyo tangu awali imeonyesha ujasiri wa kuitoa baada ya kudai inaweza kufanya kazi kwa asilimia zaidi ya 90.

Iwapo, Kampuni ya Moderna itapewa ridhaa na kuanza kuitoa mapema mwezi huu italeta matokeo chanya,kwani tayari imekamilisha kufanyia majaribio chanjo hiyo, kati ya watu 30,000 na matokeo yake yalikuwa mazuri, matokeo ambayo yanafanana na ya kampuni ya Pfizer.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news