Dada wa kazi aua kwa kisu kwa kuambiwa ana roho mbaya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, ACP Ramadhani Kingai amethibitisha kifo cha Ezekiel Nyamko aliyechomwa kisu na dada wa kazi, Happiness  nyumbani kwa rafiki yake, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kijana Nyamko mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam amechomwa kisu mara mbili kwenye kifua na mfanyakazi huyo hadi kupelekea umauti.

ACP Kingai ameeleza Novemba 30, 2020 kuwa, Ezekiel Nyamko alienda kumtembelea rafiki yake Kelvin ambaye wazazi wao pia ni marafiki.

Amesema, marehemu alipofika kama kawaida aliomba chakula, lakini mtuhumiwa alimnyima na kumwambia kuwa bado wenyeji hawajala, hivyo asubiri. Nyamko akamjibu kuwa “una roho mbaya kama sura yako” na kuongeza kuwa ndiyo maana Kelvin hakuoi".

Maneno hayo yanadaiwa yalimkera mtuhumiwa na kufikia hatua ya kumchoma kisu kifuani mara mbili.

Hata hivyo, Mtuhumiwa ameshikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi ambapo Kamanda huyo amerejea wito kwa kila mwananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news