Hawa ndiyo wafanyakazi bora Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akisoma majina ya wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo ambapo wafanyakazi watatu walichaguliwa na kupewa zawadi mbalimbali za kuwapongeza kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza George Msabila wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya cheti mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Dkt. Henry Mayala wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi laki nane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi ya cheti mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya tatu Danford Mrope wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika leo katika taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya kwanza George Msabila zawadi iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya pili Dkt. Henry Mayala zawadi iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji dawa za binadamu ya Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 aliyeshika nafasi ya tatu Danford Mrope zawadi iliyotoka kwa kampuni ya uingizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya Samiro Pharmaceutical Ltd. Kampuni ya Samiro huwa inatoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa Taasisi hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuwapa motisha ya kazi.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kurugenzi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21. Wa pili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya tatu mhasibu Danford Mrope aliyotoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia tukio la utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wa Taasisi hiyo ambapo wafanyakazi watatu walichaguliwa na kupewa zawadi mbalimbali za kuwapongeza kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi.[Picha zote na JKCI].

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news