KMC FC yaendelea kujifua kuelekea michezo ya Ligi Kuu Novemba 21 dhidi ya Azam FC

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imendelea kujifua leo kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo Zanzibar KMKM, ikiwa ni katika mikakati ya kujiimarisha kuendelea kwa michezo ya ligi kuu Soka Tanzania Bara Novemba 21 mwaka huu.

Katika mchezo huo, KMKM imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja ambapo KMC FC ilipata goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Hassan Kapalata.

Aidha mbali na mchezo huo wa leo, KMC FC hadi sasa imeshacheza michezo mitatu ya kirafiki ambayo ni dhidi ya Mbeya kwanza ambapo iliweza kutoka sare ya bila kufungana,Timu ya Benki ya DTB, ambapo KMC FC ili ibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja.

Kupitia michezo hiyo inatoa nafasi kwa walimu kuendelea kukikosa kikosi vizuri na hivyo kufanya marekebisho ili kuhakikisha kwamba katika mchezo dhidi ya Azam Novemba 21 mwaka huu timu hiyo inakwenda kupata matokeo mazuri.

Aidha bado KMC FC inauwezo mkubwa wakufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu inayoanza Jumamosi ijayo kutokana na ubora wa kikosi hicho na kwamba marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanywa na walimu na hivyo mashabiki na wapenzi wa Timu hiyo kuweza kupata burudani pamoja na ushindi kwa kila mchezo.
Imeandaliwa na Christina Mwagala.Afisa habari na mahusiano wa Timu ya KMC FC


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news