MASWALI NA MAJIBU KUHUSU TIN KWA WAAJIRIWA


1. Swali :Nini maana ya TIN?Jibu : TIN ni namba ya utambulisho wa mlipakodi.

2. Swali : kuna matumizi ya aina ngapi ya TIN?

Jibu: Kuna aina mbili ya matumizi ya TIN ambayo ni ya kibiashara na yasiyo ya kibiashara.

3. Swali: TIN huitajika kwenye malipo gani?

Jibu: Hutumika kwenye malipo ya kodi katika biashara,ajira, uwekezaji na pia katika malipo yasiyohusu kodi mfano ada ya leseni ya udereva.

4. Swali: Matumizi yasiyo ya biashara ni yapi?

Jibu: Matumizi hayo ni pamoja na ajira, umiliki wa chombo cha moto na leseni za udereva.

5. Swali: Kwa hiyo TIN inayotokana na ajira inakuwa siyo ya biashara?

Jibu : Ndiyo

6. Swali: Nini umuhimu wa jambo hili?

Jibu : Kila anayelipa kodi anapaswa kuwa na TIN kulingana na kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura 438.

7. Swali: Inamaana kodi itaongezeka ?

Jibu : Hapana, makato ya kodi yatakuwa yale yale.

8. Swali: Ikiwa mimi ninayo TIN tayari kuna haja ya kupata TIN kwa ajili ya ajira?

Jibu : Hapana TIN hiyo ya mwanzo ndio itatumika na TIN huwa ni moja kwa mtu mmoja.

9. Swali: Mimi nina leseni ya udereva TIN yangu nitaijuaje.

Jibu: Fika katika ofisi yoyote ya TRA utapata TIN yako.

10. Swali : Je taratibu za kupata TIN ni zipi?

Jibu: Ni kwa kuingia www.tra.go.tz kisha usajili wa TIN, weka namba ya NIDA na namba ya simu kisha jaza taarifa zako utapata TIN.

11. Swali: Ikiwa sina namba ya NIDA au NIN kuna utaratibu upi wa kuipata?

Jibu: Fika ofisi ya TRA na kitambulisho cha kura au barua ya serikali ya mtaa, utachukuliwa alama za vidole na kupata TIN yako.

12. Swali: TIN inapatikana kwa bei gani?

Jibu: TIN ni bure kabisa hakuna malipo yoyote.

13. Swali: kwa mtu mwenye TIN ya matumizi ya biashara anaweza akaitumia kwenye ajira?

Jibu : Ndiyo, kwa sababu TIN ya matumizi ya biashara inatumika kwenye kila jambo.

14. Swali: Nikishapata TIN nitaifanyia nini?*

Jibu : Kwa wewe mwajiriwa ipeleke kwa mwajiri wako aweze kuijaza katika taarifa ya makato ya kodi kwa waajiriwa.

15. Swali: Je kila mwajiriwa analipa kodi ya ajira?

Jibu: Mwajiriwa mwenye mapato kuanzia shilingi 270,001 na kuendelea kwa mwezi ndiye atakayekatwa kodi kutokana na ajira.

16. Swali: Kama kiwango changu cha mshahara ni chini ya shilingi 270,000 kwa mwezi ninapaswa kuwa na TIN.

Jibu: Ndiyo, Unapaswa kuwa na TIN kwa kuwa unachanzo cha mapato yanayohusu kodi ingawa hujafikia kiwango cha kutozwa kodi.

Kwa maelezo zaidi piga simu bure kwenda namba 0800780078 au 0800750075au tuma ujumbe whatsapp 0744233333 au barua pepe huduma@tra.go.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

Previous Post Next Post

International news