Mdee:Mimi na wenzangu hatutaondoka CHADEMA

"Mimi na wenzangu hatuchomoki. Niwahakikishie wana Chadema wanaosema nimenunuliwa, kuwa hatujanunuliwa, Ninasema haya kwa sababu, kumekuwa na maneno mengi. Kuna watu wanasema,"
Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 1, 2020 jijini Dar es Salaam. (Picha na Diramakini).

"Halima amenunuliuwa, niseme mimi Halima Mdee, sijawahi kununuliwa, sitarajii kununuliwa. Watu waliofanya kazi na mimi ndani ya miaka 16 iwe mgeni kwa miaka 15, wananijua. Mimi sina thamani ya kipande cha senti. kazi zangu zote nimekuwa nikifanya kwa uaminifu ndani ya chama. Mimi na wenzangu, tutaendelea kuwa wanachama waaminifu wa CHADEMA,"anasema.

"Mimi na wezangu tumechukuliwa hatua na kamati kuu, niwahakikishe, mimi na wenzangu tutabaki kuwa wana Chadema kindaki ndani. Mimi dhamira ya kuondoka Chadema haipo. Pamoja na changamoto tunayopitia, Halima mnayemfahamu miaka yote, ni yuleyule na nikisema Halima na timu yangu yote;

Wabunge wengine wa viti maalum ni Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya, Agnes Kaiza, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza.
 
"Sisi na CHADEMA ni damu damu, ndiyo maana umeona hapa tumevalia kombati. Tutaendelea kumuheshimu Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe, kuna wanaosema ambayo hawayajui,lakini tunaangalia njia bora ya kuangalia namna ya kutatua tatizo hili, hivyo tutaendelea kuwa wanachama wa hiyari, nipende kusema tunakipenda CHADEMA, tunakiheshimu CHADEMA na hatutaondoka,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news