Mwanasheria Mkuu aionya CHADEMA wabunge viti maalum

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Profesa Adelardus Kilangi amewaonya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwataka kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti maalum kutoka chama hicho.ambao waliapishwa hivi karibuni, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Wabunge hao 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameapishwa hivi karibuni katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika Job Ndugai.

Wengine ni Asia Mohamed, Felista Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Simon, Anatropia Theonest,Salome Makamba, Conchester Lwamraza, Grace Tendega, Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya,Agnes Kaiza,Nusrat Hanje,Jesca Kishoa,Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.

Prof.Kilangi amesema, mchakato wa wabunge wa Viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.
Awali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa wabunge hao wa viti maalum CHADEMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news