Mwenyekiti CCM Mara ampongeza Rais Magufuli kwa kusimamia uteuzi wa wagombea makini nafasi za Umeya, Wenyeviti

Siku chache baada ya Chama Cha Mapunduzi (CCM) kupitisha majina kadhaa ya wagombea umeya wa majiji, manispaa na uwenyekiti wa halmashauri za wilaya na miji,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye (Namba Tatu) amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kwa kusimamia vema zoezi hilo la uteuzi,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Amesema, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Dkt.Magufuli imefanya kazi nzuri, hivyo baada ya hatua nyingine kukamilika jukumu la uchaguzi waachiwe madiwani na si baadhi ya makada kupachika makundi yao.

Pia amesema, suala la rushwa halikubaliki na kila mmoja atambue kuwa, makachero wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wapo macho saa 24 huku akisisitiza pia mchakato huo haupaswi kuwagawanya madiwani.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho chini ya mwenyekiti wake, Dkt.John Magufuli aliagiza kufanya mapitio na mchujo wa wagombea wote wa nafasi hizo.

Kabla ya kutaja orodha ya majina ya wagombea wanaotakiwa kuanza kupigiwa kura Novemba 23 na 24, 2020  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho amesema kamati imefikia uamuzi huo ili kupata viongozi waadilifu, wazalendo na wachapa kazi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye amesema, hatua inayofuata sasa ni madiwani kuwachagua hivyo, mchakato huo muhimu haupaswi kuingiliwa na watu wenye maslahi binafsi.

"CCM tumekuwa waongoza njia katika demokrasia ndani na nje ya nchi. Hivyo suala la uadilifu na kutoingilia majukumu ya madiwani wakati wakiwachagua mameya na wenyeviti wa halmashauri ni jambo muhimu mno.

"Madiwani waachiwe wapige kura siku hiyo ikifika ili kupata viongozi ambao ni chaguo sahihi katika manispaa,halmashauri za wilaya na majiji," amesema Kiboye.

“Zamani mchakato wa kuwapata viongozi hawa ulifanyika ngazi ya mkoa sasa kamati kuu ikapendekeza halmashauri zote iwathibitishe kabla ya kupigiwa kura na baraza la madiwani,hivyo zoezi hili linafanyika kitaalam na ni shirikishi,"ameongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news