Naibu Kamishna wa Polisi afariki

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ametangaza kifo cha Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari kilichotokea Novemba 17, 2020 katika Hospitali ya Christian Medical Center Trust (DCMCT) iliyopo jijini Dodoma Dodoma ambako alikuwa akipatiwa matibabu, anaripoti Mwandishi Diramakini.

IGP Sirro amesema, Kamanda Dhahiri Kidavashari amefariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari.
Amesema kuwa, msiba upo Kisasa jijini humo katika nyumba 300 huku taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea.Hakika sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea, Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema. Amin.

Post a Comment

0 Comments