Rais Dkt.Mwinyi awataka mawaziri kuwa na nyaraka tano

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameainisha aina tano za nyaraka ambazo amesema ni lazima kila waziri awe nazo ili kuwezesha Serikali yake kufikia malengo ya haraka kuwaletea maendeleo wananchi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ameyabainisha hayo leo Novemba 21, 2020 ikiwa ni mwendelezo wa hatua kabambe alizonazo za kuhakikisha kuwa kauli mbiu yake ya Yajayo Yanafurahisha inafikiwa kikamilifu.

"Nyaraka zifuatazo lazima Mawaziri wawe nazo kwa ajili ya kutengeneza mpango kazi. Mosi ni kila Waziri anapaswa kuwa na Ilani ya Uchaguzi na kufahamu inasema nini juu ya wizara yako.
"Pili hotuba yangu ya ufunguzi wa Baraza la Wawakilishi inakuelekeza nini katika wizara yako. Tatu ahadi zangu wakati wa kampeni zinasemaje. Mawaziri watapewa kitabu kutoka ofisi yangu chenye ahadi zangu wakati wa kampeni.

"Suala la nne ni mawaziri wapate maoni ya wadau katika wizara. Tano ni Dira ya Maendeleo iwe kigezo katika mpango kazi wako.Mpango kazi uwe na bajeti, wataalam wanatuambia mpango bila bajeti ni Rasimu sio mpango, tunataka mpango wenye bajeti utakaotuonyesha wazi nini tunatakiwa kufanya, kina gharama gani ili tuweze kuweka kwenye bajeti tutekeleze mara moja,"amefafanua Rais Dkt. Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news