Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja kuhusu ajira mpya za walimu

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za walimu, anaripoti Angela Msimbira (OR-TAMISEMI).
Ufafanuzi huo umetolewa leo Novemba 30, 2020 katika Ofisi ya Rais-TAMISEMI jijini Dodoma mara baada kutokea hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu ajira mpya za walimu zilizotangazwa hivi karibuni. 

Amesema, ajira hizo zilitangazwa baada ya kukamilia kwa mchakato wa uchambuzi wa maombi ya ajira uliofanywa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Tume ya Utumishi wa Walimu.

Mhandisi Nyamhanga amesema, hoja kubwa ilyojitokeza ni kwa jina la Mwalimu mmoja kujitokeza katika kila ukurasa na kuonekana mara 196, badala ya mstari wa maelezo ya Jedwali (Sub- titles) lakini shule aliyopangiwa ni moja, pamoja na jina hilo kujirudia halikuchukua nafasi ya mwombaji yoyote ya walimu waliotakiwa kuajiriwa au kuathiri idadi ya walimu waliotakiwa kuajiriwa na tayari marekebisho yamefanyika.

Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa, shule binafsi kupangiwa mwalimu, Serikali imekuwa ikiingia ubia na baadhi ya shule binafsi ambazo hupokea wanafunzi wenye uhitaji maalum, shule hizo hupamgiwa walimu na kupewa ruzuku ya uendeshaji hivyo Shule ya Mwalimu Tutuba ilikuwa katika mchakato wa kuingia ubia na serikali lakini haukukamilika, hivyo Serikali baada ya kujiridhisha mwalimu aliyepangiwa katika shule hiyo amepangiwa katika Shule ya Sekondari Malagarasi. 

Kwa upande wa wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017, 2018 na 2019 kupangiwa vituo vya kazi Mhandisi Nyamhanga ameeleza,  waombaji wa ajira walitumia mwaka wa kuhitimu chuo badala ya mwaka wa kuhitimu kidato cha nne ambapo waombaji 27 waliandika mwaka 2019, waombaji 27 waliandika mwaka 2019 na waombaji 13 waliandika mwaka 2017, Serikali ilihakiki vyeti vyao na kubaini kuwa waombaji hao walihitimu kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

Kwa kuongezea amesema kuwa, Serikali imefuata utaratibu wa kuhakikisha waombaji wote waliopata nafasi ya ajira wanazingatia vigezo vilivyotolewa katika tangazo la ajira ambapo lilifafanua kuwa mwombaji asizidi umri wa miaka 45.

Aidha, Mhandisi Nyamhanga amewalekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakiki vyeti halisi vya waliopata ajira na kujiridhisha kabla ya kutoa barua za ajira, na kusisitiza kuwa endapo itabainika udanganyifu au kasoro za vyeti vya kitaaluma wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema Serikali imetoa ajira za walimu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza wametoa ajira 8000 na awamu ya pili watatoa kwa walimu 5000 ili kupunguza malimbikizo ya mshahara kwa walimu wapya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameweka wazi kuwa Serikali itahakikisha walimu wote waliomba ajira kwa masomo waliyoomba yanaendana na masomo wanayoyafundisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news