Simba yaichapa Plateau United 1-0

Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa alama tatu muhimu baada ya kuitwanga bao moja timu ya Plateau United bao 1-0 katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika katika hatua ya awali, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, bao pekee la Clatous Chama alilolipachika nyavuni dakika ya 53 ndilo lililodumu hadi dakika ya mwisho. 
 
Katika mtanange huo ambao umepigwa katika uwanja wa Rwang Pam Stadium Stadium uliopo Jos, Nigeria unaifanya Simba SC kujiwekea mazingira mazuri hatua inayofuata.

No comments

Powered by Blogger.