Tanzanite yatwaa ubingwa wa COSAFA


Timu ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania imeibuka mshindi wa mashindano ya COSAFA 2020 baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 4-3 katika Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini, mchana huu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
Zambia ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema kunako kipindi cha kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Comfort Selemani ambalo lilidumu mpaka kipindi cha pili dakika ya 90.
Mwamuzi aliongeza dakika tano kufidia muda uliopotea katika matukio mbalimbali ambapo dakika ya 90+4′ Tanzania ilipata penati baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya penati boksi. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha kupitia penati hiyo iliyopigwa na Koku Kipanga mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania 1-1 Zambia.
Miamba hao walitengewa matuta ambapo Tanzania aliibuka na ushindi wa penati 4-3 na kutawazwa kuwa mabingwa wa COSAFA Women Championship. Tanzania imeingia kama timu mwalikwa katika michuano hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news