Uganda yagundua tiba ya Corona

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema kwamba, wanasayansi nchini humo wamepiga hatua kubwa katika kupata tiba dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Corona (COVID-19),anaripoti Mwandishi Diramakini.

"Wanasayansi wetu wameniambia habari njema kwamba wameunda dawa saba tofauti. Sita kati ya hizo zinafanyiwa majaribio na moja inaongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona. Dawa za kwanza tatu zinauwa virusi hivyo na kuzuia uharibifu mwilni;

Museveni ameyasema hayo Novemba 29, 2020 wakati akihutubia Taifa kupitia runinga ambapo amesema kwamba,wanasayansi nchini humo wamefanyia majaribio tiba hiyo ambayo hakutoa maelezo zaidi.

Amesema kuwa,kwa sasa, madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini dhidi ya virusi vya COVID-19.

Rais Museveni amesema kwamba, dawa hiyo imefanyiwa majaribio kwa wagonjwa kadhaa wa Corona na kupona na itaanza kutumika kwa watu wote kuanzia Desemba 15, 2020.

Amesema, katika muda wa siku 40, dawa hiyo itakuwa imetibu watu wengi huku akisisitiza kuwa, mafanikio hayo ni hatua njema kwa Taifa hilo la Afrika Mashariki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news