Wanafunzi 490,103 kufanya Mitihani ya Kidato cha Nne leo

Wanafunzi 490,103 leo Novemba 23, 2020 wanatarajiwa kufanya Mitihani ya Kidato cha Nne ambapo kati yao wavulana ni 213,553 sawa na asilimia 47 huku wasichana wakiwa ni 234,103 sawa na asilimia 52.3, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kati ya wanaotarajiwa kufanya mitihani hiyo watahiniwa binafsi ni 41,939 wavulana wakiwa 18,118 sawa na asilimia 43.2 na wasichana ni 23,821 sawa na asilimia 56.8.

Pia wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 893 ambapo 425 kati yao ni wenye uoni hafifu, 60 wasioona, 186 viziwi na 222 walemavu wa viungo.

Katika kundi la watahiniwa binafsi wanafunzi wenye mahitaji maalum kwenye kundi hilo ni 11 ambapo saba kati yao wana uoni hafifu na wanne ni wasioona.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka 2019 wanafunzi waliofanya Mitihani ya Kidato cha nne walikuwa ni 485,866, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 0.9.

Hata hivyo, kuhusu Mtihani wa Maarifa (QT) jumla ya wanafunzi 9,426 wanatarajiwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 4,147 sawa na asilimia 44 na wasichana ni 5,279 sawa na asilimia 56 ambapo katika kundi hili waliofanya mwaka 2019 ni 12,984 hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news