Benki ya Equity yazindua VISA USD Debit Card kurahisisha manunuzi

Taasisi inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kifedha, Equity Bank Limited, leo Desemba 2, 2020 imezindua kadi mpya ya kisasa ya Visa inayotumia mfumo wa sarafu ya Dola ya Kimarekani ‘VISA USD Debit Card’ kwa ajili ya matumizi ya wateja wake nchini Tanzania, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Meneja Huduma Mbadala za Benki wa Benki ya Equity, Magreth Mwasumbi (kushoto), Meneja Diaspora wa Benki ya Equity, Doreen Raphael (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Teknolojia ya Hanari na Mawasiliano (TEHAMA), Keneth Wakati wakionesha mfano wa kadi hizo mara baada ya kuzindua.

Dondoo Muhimu

*Pamoja na kutumika katika mashine mbalimbali za kutolea fedha (ATM), wateja wataweza kufanya manunuzi katika duka lolote linalotumia kadi hiyo ya Visa, kama vile Maduka makubwa ya bidhaa (supermarkets), migahawa, hoteli, sehemu za hosptali na vituo vya mafuta, maduka ya kawaida n.k.
 
*Wateja watafanya manunuzi kupitia mtandaoni pasipo na gharama yoyote ya ziada.
 
*VISA USD Debit Card itampa mteja fursa ya kufanya manunuzi kwa sarafu ya Dola ya Kimarekani bila kuingia gharama yoyote za ziada

*Kadi hii ni ya kwanza na ya kipekee katika soko nchini Tanzania.

*Inatumia mfumo wa chip na neno la siri kwaajili ya usalama na ubora kwa mtumiaji.

*Kadi hii inatumia mfumo PayWave unaompa mtumiaji fursa ya kufanya miamala ya manunuzi madogomadogo wakati wote.
Meneja Huduma Mbadala za Benki wa Benki ya Equity, Magreth Mwasumbi (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo Desemba 2, 2020 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kadi za kutoa fedha za kigeni (Visa debit card) ambapo mteja akiwa na kadi hiyo ana uwezo wa kufanya malipo katika maduka makubwa na madogo, migahawa, hospitali, vituo vya mafuta, hotelini na huduma nyingine nyingi. Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wengine pichani kushoto ni Meneja Diaspora wa Benki ya Equity, Doreen Raphael pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),Keneth Wakati.

Kadi hiyo iliyotengenezwa kwa kiwango cha dhahabu ni ya kwanza na ya kipekee ikiwa na malengo ya kutoa urahisi na upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, ambao wanataka kufanya manunuzi kupitia mtandaoni au kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya Dola ya Kimarekani.

Kadi hiyo inampa mteja fursa ya kulipia bidhaa na huduma mbalimbali kwa sarafu ya Dola ya Kimarekani pasipo nyongeza ya malipo yoyote ya ziada. Pia itamsaidia mteja kufanya miamala pasipo kuvuruga bajeti yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania Limited, Robert Kiboti amesema kuwa, kadi hiyo ni nafuu, inatoa suluhisho la bei, ni rahisi na salama kwa mteja na itamsaidia sana mteja katika kurahisisha huduma kwa wakati sahihi, lakini pia kuchochea ukuaji wa biashara ya mtandaoni.

“Kadi ya Visa Gold Debit inaruhusu wateja kulipia bidhaa au huduma kwa Dola za Kimarekani kwa viwango vilivyoonyeshwa kwa wakati huo. Hii inamaanisha kuwa ikiwa unalipa bidhaa inayouzwa Dola 10 za Kimarekani, hiyo ndiyo inayokatwa katika akaunti yako, hakuna malipo mengine, ”anasema Kiboti

“VISA USD Debit Card inatumia mfumo wa PayWave ambapo pia mtumiaji ana uwezo wa kufanya manunuzi madogomadogo,” Mkurugenzi Mkuu, Bw.Kiboti amefafanua zaidi.

Visa PayWave ni teknolojia ya malipo isiyohusisha mawasiliano ya moja kwa moja isipokuwa kupitia mawasiliano ya kimtandao kwa kutumia chip maalumu yenye ili mtumiaji kupokea malipo.

“Kadi hii inatumia mfumo wa chip na neno la siri kwa ajili ya usalama na ubora kwa mtumiaji,” ameeleza Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Keneth Wakati.

Uzinduzi huo unakuja kufuatia mwenendo wa mabadiliko ya biashara ya kielektroniki, wakati ambao biashara nyingi zinahamia katika mtandao, ikiwa ni mojawapo ya madhara ya mlipuko wa Covid-19.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news