Biharamulo yakabiliwa na upungufu vyumba 64 vya madarasa

Zaidi ya wanafunzi 15,000 wanatarajiwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza katika Halmashauri ya Wilaya Biharamulo mkoani Kagera huku upungufu wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo ukiwa ni vyumba 64, hali inayoweza kusababisha kuwepo kwa mrundikano wa wananfunzi kwenye vyumba vya madarasa vilivyopo,anaripoti Allawi Kaboyo.

Mifuko ya saruji iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesaa pamoja na Mwenyekititi wa UWT Mkoa wa Kagera ikishushwa katika ofisi za Halmashauri ya  Wilaya Biharamulo. (Picha na Diramakini).

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Waziri za Kombo ameyasema hayo Desemba 1, 2020 kwenye hafla ya kupokea mchango wa wadau wa maendeleo iliyofanyika katika ofisi za mkurugenzi na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya hiyo.

Waziri Kombo amesema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo ina changamoto kubwa kwenye miundombinu ya shule hasa upande wa sekondari.

Mkuu wa Wilaya Biharamulo, Kanali Mathias Kahabi akizungumza katika hafla ya kukabidhi mifuko 300  ya saruji kwa ajili  ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Biharamulo. (Picha na Diramakini).

Amesema kuwa, halmashauri hiyo inazo shule za sekondari 20 za serikali ambazo wanafunzi hao waliofahulu elimu ya msingi wanatakiwa kupokelewa na kuongeza kuwa idadi ya wananfunzi wanaoondoka kwa maana ya kidato cha nne ni wachache ukilinganisha na wanaoingia kwa kidato cha kwanza hali inayopelekea kuwepo kwa mapungufu hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhe.Mhandisi Ezra Chiwelesa ambaye amekebidhi mifuko 200 ya saruji katika kuwezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa amesema kuwa, mchango huo ni wa awali kadiri muda unavyozidi kwenda ataweza kuleta michango mingi zaidi kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kagera na Mkurugenzi wa Kampuni ya Samudi Investment,Hajat Faidha Kainamula akizungumza katika hafla ya kukabidhi mifuko 100  ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Biharamulo. (Picha na Diramakini).

Amesema kuwa, Biharamulo itaweza kujengwa na Wananbiharamulo wenyewe ambapo ametoa wito kwa jamii nzima kuliona hili kuwa ni la kwao na kuweza kushiriki kikamilifu huku akimtaka mwenyekiti mteule wa halmashauri kuwahimiza madiwani wake kuwahusisha wananchi kwenye hili ili mwakani watoto wanapoanza shule changamoto hiyo iwe imekwisha.

“Nilipokea barua kutoka kwa mkurugenzi ikiniomba kuchangia kama mdau lakini kama kiongozi, namimi kwa kuliona tatizo hili kwa umuhimu wake maana nimepita kwenye maeneo yote ya wilaya hii nimejionea hali ilivyo, ndio maana nimeamua kwa haraka kuleta hii saruji ili iweze kusaidia maana januari watoto wanatakiwa kuanza masomo,amesema Mhe.Chiwelesa.

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhe. Mhandisi Ezra John Chiwelesa aliyesimama akizungumza katika hafla ya kukabidhi mifuko 200  ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Biharamulo. (Picha na Diramakini).

Hajat Faidha Kainamula ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa wa Kagera (UWT) yeye kama mdau wa maendeleo amekabidhi mifuko 100 ya saruji ambapo mifuko 50 ni kutoka kwenye kampuni yake ya SAMUDI INVESTMENT na mifuko mingine 50 ni kutoka UWT, ambapo amewataka akina mama katika maeneo yao kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanawezesha ujenzi wa madarasa hayo.

Bi Kainamula ameongeza kuwa, amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa miaka mingi hivyo anajua changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu ambapo ametoa wito kwa wanannchi wote wa Biharamulo kuhakikisha wananchangia madarasa hayo.
Wadau wa maendeleo ambao ni Mbunge wa Jimbo la Biharamuo Magharibi, Mhe.Mhandisi Ezra Chiwelesa wa tatu kulia pamoja na Mwenyekiti wa  UWT Mkoa wa Kagera, Hajat Faidha Kainamula wa pili kushoto wakikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Kanali Mathias Kahabi wa tatu kushoto pamoja na viongozi wengine.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo mkuu wa wilaya Biharamulo, Kanali Mathias Kahabi amewashukuru wadau hao kwa mchango wao mkubwa katika halmashauri hiyo huku akimsifu Mhe. Mbunge kwa namna alivyoanza kutekeleza ahadi zake kwa kipindi kifupi na kwa haraka tofauti na watu walivyodhani.

Kahabi amesema kuwa, wilaya hiyo imekuwa ikishindwa kwenda mbele kutokana na kuwepo kwa wapigaji wengi na sasa hali hiyo imeanza kupotea kutokana na uwepo wa viongozi madhubuti na kuwataka watumishi kutojisahau katika utumishi wao na badala yake wajikite katika kutatua kero za wananchi.

Amesema kuwa, msaada huo umekuwa chachu kubwa ya maendeleo na mfano mkubwa wa kuigwa kwa wadau wengine maana tayari mbunge kaonyesha njia hivyo na wadau wengine wanatakiwa kufata nyayo hizo ili kuweza kuibadirisha Biharamulo na kuweza kuendana na kasi iliyopo ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news