Bilionea wa Urusi akutwa amefia hotelini Zanzibar

Bilionea kutoka nchini Urusi, Igor Sosin amekutwa akiwa amefariki dunia wakati akiwa kwenye mapumziko na binti yake Taisia katika hoteli ya Park Hyatt Mji Mkongwe visiwani Zanzibar. 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amesema bilionea huyo alikuwa na mwanamke aliyejulikana kwa jina la Arafa Ramadhani Mpondo (23) mkazi wa Fuoni ambaye anadaiwa ni mpenzi wake aliyempata mtandaoni. 

Hata hivyo, chanzo cha kifo chake bado hakijabainishwa, lakini miezi kadhaa iliyopita aliugua virusi vya Corona (COVID-19) ambapo baadae ilidaiwa alipona.

Post a Comment

0 Comments