BRELA yatoa tahadhari kuhusu makampuni ambayo hayajahuisha taarifa

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)unapenda kutoa tahadhari kwa Wizara, Mamlaka, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi na Umma kwa ujumla kuhusu uwepo wa makampuni ambayo hayajahuisha (update) taarifa zake kwa mujibu wa sheria. 

Kwa taarifa hii,umma unahimizwa kuhakikisha mikataba yote ya manunuzi ya vifaa au huduma (all kinds of contractual transactions) baina yao na kampuni binafsi isainiwe baada ya kujiridhisha kwamba kampuni husika imehuisha taarifa zake za mwaka katika Daftari la Makampuni kama yalivyo matakwa ya Sheria na kama kampuni hizo bado ziko hai.

Kujiridhisha huko kufanyike kwa kampuni husika kutakiwa kuwasilisha Cheti cha Usajili (Certificate of Incorparation) na nakala ya Mizania yake ya Mwaka huo (Annual returns) iliyoidhinishwa na Msajili wa Makampuni au Taarifa Rasmi (Official Search Report) iliyosainiwa na Msajili wa Makampuni.No comments

Powered by Blogger.