Chalinze yafanya tathimini ya lishe

Kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe katika Halmashauri ya Chalinze kimefanyika jana katika Ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugoba,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kikao hicho kilijumuisha wajumbe wa kamati ya lishe wilaya, watendaji wa vijiji na kata na wenyeviti wa vitongoji. 
Mkataba wa lishe ni mkataba kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na watendaji wa kata, watendaji wa kata na watendaji wa vijiji. Mkataba huo ni mkataba wa usimamizi bora lishe Katika Halmashauri ya Chalinze.

Katika tathimini hiyo ya mkataba wa lishe, mkataba huo umetekelezwa vizuri na unaendelea kutekelezwa kwa umakini mkubwa. Wajumbe waliupitia mkataba wa lishe na kuona baadhi ya kata zilizofanya vizuri katika utekelezaji wa mkataba huo.Kata zilizofanya vizuri ni kata ya Msata na Msoga.

Kata hizo zimetekeleza viashiria vya mkataba wa lishe vizuri ukilinganisha na kata zingine ndani ya Halmashauri ya Chalinze na kikao cha Tathimini kiliwapongeza na kuzitaka kata zingine kuiga mfano wa kata zilizotekeleza vema.

Aidha, katika kikao hicho cha tathimini iliwekwa mikakati mbalimbali ya kutokomeza Tatizo la utapiamlo Katika jamii ya wana Chalinze.

Post a Comment

0 Comments