Dkt.Mkamilo: TARI imeweka mikakati thabiti kuongeza ufanisi

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI ) imeweka mikakati thabiti kuhakikisha kuwa inawaondolea kero zinazowakabili watumishi wake ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, anaripoti Sankana Simkoko (TARI Mlingano).

Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt.Geofrey Mkamilo ameyabainisha hayo wakati akizungumza na watumishi wa Kituo cha TARI Mlingano alipofanya ziara ya kushitukiza kuona na kukagua shughuli za kila za kituo.

Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt. Geofrey Mkamilo akiaaangalia sampuli ya udongo katika Maabara Kuu ya Taifa ya Upimaji wa udongo liliyopo Kituo cha Utafiti wa Kilimo Mlingano.

“TARI itahakikishia kuwa inajitahidi kuondoa kero zinazowakabili watumishi wote wa taasisi hiyo ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku,"amesisitiza Dkt.Mkamilo katika mazungumzo yake wakati akijibu malalamiko yaliyoibuliwa na watumishi wa kituo katika kikao hicho.

Baadhi kero zilizoibuliwa na watumishi ni pamoja na stahiki za malipo ya likizo, uchakavu wa ofisi na nyumba za watumishi na madai ya nyongeza za mishahara baada ya kupandishwa vyeo vipya.

Kuhusu uchakavu wa ofisi na nyumba alisema, Serikali imeweka mpango ambao utawezesha kufanya ukarabati kwa awamu ili kuendana na fedha zitakazopatikana katika bajeti.

Jambo lingine ambalo ni faraja kwa watumishi aliloligusia Dkt.Mkamilo ni muundo wa utumishi wa TARI unafanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika na ukiwa tayari watumishi watatarifiwa rasmi.

Kuhusu vietendea kazi katika Maabara Kuu ya Taifa ya Upimaji Udongo iliyopo TARI Mlingano, Dkt.Mkamilo aliwahakikishia watumishi hao kuwa vifaa vitapatatikana na vingine vilivyopo vitatengenezwa kwa gharama yoyote ili kufikia malengo yaliyowekwa na maabara hiyo kubwa kuliko zote nchini zinazopima afya ya udongo na mimea.

Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt. Geofrey Mkamilo akikagua shamba la mbegu bora ya zao la mkonge lililopo Kituo cha Utafiti wa Kilimo Mlingano.

Pia amewataka watafiti wa kituo hicho kuthubutu kuandika maandiko ili kuweza kupata miradi itakayoweza kukiingizia kituo fedha na pia kuinua Sekta ya Kilimo hapa nchini kupitia tafiti zao.

Dkt.Mkamilo amesema, TARI imejipanga kuhakikisha kuwa kero ndogondogo zinazowakabili watumishi wote wa zinaondolewa haraka ili kuleta motisha kwa watumishi na kuwawezesha kuchapa kazi kwa bidii.

TARI imepewa majukumu na Serikali kufufua na kuendeleza mazao mbalimbali nchini likiwemo zao la mkonge ikiwa ni maagizo yalitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea kituo cha TARI Mlingano hapo Juni 1, 2019.

TARI Mlingano imepewa jukumu la kitaifa kushiriki kikamilifu katika kufufua zao la mkonge kupitia tafiti, mafunzo kwa wadau wa mkonge na uzalishaji wa mbegu bora za mkonge.

Hivyo kutokana na jukumu la kituo cha TARI Mlingano, Dkt.Mkamilo amewataka watumishi hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuweza kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Serikali kupitia Mheshimiwa Majaliwa ili kuweza kurudisha hadhi na mchango wa zao la mkonge kwa uchumi wa Taifa.

“Tupo kwa ajili ya kazi tutumie muda wetu wa kazi kufanya kazi kwa bidii zote na uwezo tulionao kwani Serikali yetu ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli ina mipango mizuri ya kusasaidia shughuli za utafiti wa kilimo hapa nchini,"ameongeza Dkt.Mkamilio.

Kutokana juhudi mpya zilizoibuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano tayari mikoa kadhaa imeamua kufufua au kuanzisha kilimo bora cha mkonge, mikoa hiyo ni Tanga, Morogoro na Kilimanjaro.

Mikoa mingine iliyoonyesha nia ya dhati kuinua la kufanya zao la mkonge kuwa la kibiashara ni Shinyanga, Simiyu, Mara, Pwani and Lindi wamepata mafunzo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news