Dkt.Sengati atoa siku 14 maji yarudishwe Soko Kuu Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha wamerudisha maji katika Soko Kuu, anaripoti Tiganya Vicent (RS) Tabora.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kukagua masoko ya Tabora kwa ajili ya kujionea matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo wafanyabiashara.

Dkt. Sengati alichukua hatua hiyo baada ya kutembelea soko kuu wa kukuta maji yamekatwa na wafanyabiashara wa soko hilo wakiendesha shughuli zao bila ya kuwa na maji ya uhakika.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Philemon Sengati akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara wa soko kuu na wale wa Kachoma wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira sokoni hapo.

“Nataka hapa watu wapate maji ya uhakika ndani ya wiki mbili …angalie katika ‘strategic area’ muweke maeneo ya watu kupata maji ambayo yatawasaidia kufanya biashara zake bila matatizo,” amesema.

Dkt.Sengati amesema, utatuzi wa tatizo la maji katika soko hilo na mengine lazima ufanyike haraka ili kulinda afya za wafanyabiashara hao. 

Mkuu huyo wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kukutana na viongozi wa masoko ili kuweka mpango wa endelevu wa kuhakikisha maji hayakatwi na Mamlaka ya Maji kwa sababu ya watumiaji kushindwa kulipia bili.

Katika hatua nyingine, Dkt. Sengati ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanaweka umeme na kuziba nyufa katika paa katika Soko Kuu na soko la Kachoma kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wa bidhaa za wafanyabiashara hao katika masoko hayo.

Amesema, uongozi wa Manispaa utakaliwa mpango wa muda mfupi wa kuhakikisha unaondoa mapungufu yaliyojitokeza katika soko la Kuu na soko la Kachoma kwa ajili ya kuwawekea mazingira mzuri ya wafanyabishara hao kufanya biashara zao katika mazingira rafiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news