FC Platinum yaichapa Simba SC 1-0, Kocha afunguka

Simba SC wameanza kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya FC Platinum kwenye mchezo wa hatua ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe jijini Harare, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Wekundu hao ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kilishuhudia bao la kwanza likifungwa na Perfect Chikwende dakika ya 17 baada ya mabeki kufanya makosa ya kumuacha nyota huyo awapite.

Aidha, mbali ya jitihada walizofanya Simba kuweka usawa mzani bao hilo kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa kuwa hawakufanikiwa kurejea katika reli.

Bao la Chris Mugalu dakika ya 78 lilitaka kuwarudisha kwenye reli ila mwamuzi alikataa kwa kueleza kuwa mfungaji alikuwa ameotea. Kupoteza mchezo wa kwanza, Simba ina deni la mabao zaidi ya mawili Uwanja wa Mkapa Januari 5, 2021 jijini Dar es Salaam

Hata hivyo, baada ya mtanange huo ambao umeonekana kuwakasirisha mashabiki wa klabu ya Simba waliokuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja naye kocha mkuu ameonyesha kutoyafurahia matokeo.

"Sijafurahia matokeo sababu hakutustahili kupoteza, tulitawala mchezo na hasa mwanzoni, lakini tulikosa umakini kwenye eneo la mwisho ili kufunga. Wamefanikiwa kufunga na hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi kwenye mchezo wa marudiano,"amesema Kocha Mkuu wa Simba, Sven baada ya mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments