Rais Magufuli ateua Mawaziri leo Desemba 5, 2020

Leo Desemba 5, 2020 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, John W. H. Kijazi ametangaza Baraza la Mawaziri baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Balozi Kijazi akitangaza Baraza la Mawaziri hao leo Ikulu, Chamwino jijini Dodoma amesema, Rais Dkt.Magufuli amewateua wafuatao kuwa mawaziri wateule akiwemo;
 
1:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Elias John Kwandikwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

2:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchika kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

3:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

4:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jumaa Hamidu Aweso kuwa Waziri wa Maji.

5:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

6:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jenister Joakim Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

7:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

8:Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) aliyekuwa akishughulikia Afya, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

9:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji)

10:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

11:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

12:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

13:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

14:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Selemani Saidi Jafo kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

15:Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Medard Matogolo Kalemani kuwa Waziri wa Nishati.

16:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Leonard Chamuriho kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

17:Mhandisi Chamuriho ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi, pia ameteuliwa na Mhe. Rais Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

18:Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Adolf Faustine Mkenda kuwa Waziri wa Kilimo.

19:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Waziri wa Madini.

20:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

21:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. George Boniface Taguluvala Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

22:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Ally Mwalimu kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

23:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Tayari Mhe. Rais Magufuli alishawateua na kuwaapisha Waheshimiwa Mawaziri 2 ambao ni Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango na Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 Wateule wote kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa wataapishwa wiki ijayo jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news