HOPE FOR GIRLS AND WOMEN TANZANIA LAOKOA WASICHANA 107 DHIDI YA UKEKETAJI MKOANI MARA

NA FRESHA KINASA

Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania (HGWT) linalojihusisha na kutoa hifadhi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji na ndoa za utotoni katika Wilaya ya Serengeti na Butiama mkoani Mara, limesema zaidi ya wasichana 107 wapya waliokuwa katika hatari ya kukeketwa limewaokoa baada ya kukimbia ukeketaji kutoka katika familia zao na kupewa hifadhi Nyumba Salama Kiabakari na Nyumba ya Matumaini Mugumu wilayani Serengeti, vituo ambavyo vinamilikiwa na shirika hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Samwelly akiwa na baadhi ya wasichana wa Kituo Cha Nyumba ya Matumaini Mugumu Serengeti, kituo hicho kinamilikiwa na shirika hilo ambacho hutoa hifadhi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji na ndoa za utotoni. (Picha na DIRAMAKINI).

Mkurugenzi wa shirika hilo, Rhobi Samwely amesema, miogoni mwao wamo waliofanya mitihani ya darasa la nne, waliohitimu darasa la saba pamoja na waliofanya mitihani ya Taifa ya kidato cha pilisi.

Amesisitiza kuwa, juhudi za kupambana na vitendo vya ukatili hususan ukeketaji vinaendelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali hasa mwezi huu wa Desemba ambao ukeketaji hufanyika kwa kiwango kikubwa.

Rhobi amesem,katika mapambano hayo, shirika limedhamiria kwa dhati kuwashirikisha wanaume, vijana na jamii kwa ujumla kujadiliana juu ya kufanya mapambano shirikishi ili kumaliza vitendo hivyo ambavyo bado vinafanywa Katika jamii ikiwemo kutoa elimu na kupokea mapendekezo yao yatakayosaidia kumaliza ukeketaji

"Lazima tushirikiane kumaliza ukeketaji, tutatumia mikutano ya hadhara kuelimisha jamii, Vijana na Wazee wa kimila katika maeneo mbalimbali ya Serengeti na Butiama lengo ni kupata ufumbuzi thabiti kutoka kwa wanaume na vijana watuambie nini kifanyike kumaliza ukeketaji, kwani kwa Sheria za Nchi ni kosa na ni kinyume pia cha haki za binadamu n hata Kitabu Kitakatifu vya Mungu (Biblia) kimezuia Uuatili " amesema Rhobi.

Amepongeza kuwa, Shirika hilo litashiriki kwa ufanisi kwa njia ya maandamano kwa siku ya kilele cha sikube 16 za kupinga Uukatili,ambapo mabinti waliopo kituo Cha Nyumba salama Kiabakari watabeba mabango yenye jumbe mbalimbali zinazoonesha kupinga Ukatili wa Kijinsia ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni katika Wilaya ya Butiama Nyumba salama kilichopo Kiabakari ili elimu hiyo iwafikie wananchi na kuwa chachu ya kufanya mabadiliko ya kuachana na vitendo vya Ukatili na badala yake watoto wa kike wathaminiwe na kupewa fursa ya elimu kwa manufaa yao na Taifa kwa siku za usoni.

"Ukeketaji unamadhara ikiwemo kutokwa damu nyingi binti anapokeketwa, maumivu makali, hatari ya kupata Magonjwa ya kuambukiza ikiwemo UKIMWI, kukatishwa masomo ili kuozeshwa, madhara ya kisaikoloji kutokana na binti kulazimishwa kukeketwa, lazima tuwahurumie watoto wa kike na kutowafanyia Ukatili huo ni jukumu la kila mmoja kuwalinda na kuwafichua wanaofanya ukeketaji kwa Siri hatua Kali zichukuliwe dhidi yao"amesema Rhobi.

Kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa (HGWT) Rhobi Samweli amesema Shirika limeweza kuokoa Wasichana zaidi ya 1,000 waliokuwa Katika hatari ya kukeketwa kupitia vituo vyake vya Nyumba salama Kiabakari Butiama na Nyumba ya Matumaini Mugumu Serengeti, Na pia limeweza kuwaendeleza kitaaluma na Kifani wasichana kutoka sehemu mbalimbali za Wilaya hizo ambao ndoto zao zingeshindwa kutimilika kwa kukatishwa masomo yao ili waozeshwe.

Rhobi Samwelly amepata kutunukiwa tuzo ya heshima ya Malkia wa nguvu kufuatia juhudi zake thabiti za kutetea wasichana dhidi ya vitendo vya Ukatili ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni,kutetea haki za Wanawake Katika kuhakikisha kwamba jamii inathamini utu, haki na heshima pamoja na kulinda haki za binadamu na misingi yake Kama ambavyo Sheria ya Nchi imeelekeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news