Jaji Harold Nsekela afariki

Harold Nsekela ambaye alizaliwa Oktoba 21,1944 na ambaye ni Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma amefariki dunia leo Desemba 6, 2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Jaji Harold Nsekela enzi za uhai wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter amethibitisha kifo hicho na kutuma salamu za rambirambi kwa familia yake.“Nimesikitishwa na kifo cha Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. Poleni familia, watumishi wote wa Sekretarieti ya Maadili na Mahakama.

"Jaji Mstaafu Nsekela alikuwa mwadilifu, mzalendo, asiyejikweza na mchapakazi. Mungu amweke mahali pema,”amefafanua Rais kupitia ukurasa wake huo.

Aidha, marehemu Jaji Nsekela aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwezi Februari, mwaka 2003 na baadaye kuteuliwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania nafasi aliyoitumikia mpaka alipostaafu kwa mujibu wa sheria.

Wakati huo huo, marehemu Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Desemba 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki leo ambapo kifo chake kimetokea jijini jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Post a Comment

0 Comments