Kada wa CCM Egla Mamoto afariki

Aliyewahi kuwa Kaimu Katibu idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Egla Mamoto amefariki dunia, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Aliyekuwa kada wa CCM, Egla Mamoto enzi za uhai wake. (Picha na Maktaba).

Mamoto ambaye katika uchaguzi wa mwaka huu aligombea ubunge kupitia kundi la wazazi, amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya usiku wa kuamkia leo Desemba 27, 2020.

Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa, Leonard Singo ametoa taarifa iliyoeleza kuwa Mamoto aliugua ghafla.

Singo amesema, marehemu alikuwa hazina katika kipindi cha uhai wake na kuwa hakupenda kuona CCM kinashindwa katika uchaguzi wowote.


Katika uhai wake alikaimu Katibu wa Uhamasishaji Taifa katika kipindi cha mwaka mmoja 2015/16 ambapo katika kipindi hicho alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana wa UVCCM.

Post a Comment

0 Comments