Katibu Mtendaji BASATA Godfrey Mungereza afariki

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza amefariki leo jijini Dodoma,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Hayo yamethibithishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi leo

“Ni kweli (Katibu Godfrey Mungereza) alikua amelazwa hospitali hamna mwenye taarifa za ziada hadi sasa, ni kweli amefia Hospitali na alikua anaumwa hata muda mimi sijui, mwenyewe nimeshtushwa,”amesema Dkt.Abbasi.

Kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali..."Nimelazwa General hapa Dom ila kila kitu kitaenda sawa kuhusu tamasha. Napambana,"ni meseji ya mwisho niliyoipokea juzi Jumanne saa tano na dakika 2 usiku kutoka kwa kaka yangu Godfrey Mungereza, Katibu Mtendaji wa BASATA, leo hatunaye tena katika dunia hii. Ametutoka.Tumwombee sana, Mola ampe pumziko la amani la milele.

Post a Comment

0 Comments