KMC FC kuwafuata Mtibwa Sugar Morogoro

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kesho itaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Ijumaa ya Desemba 11 katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo hadi sasa kimefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kipo tayari kwa mtanange huo na hivyo kuhakikisha kwamba kinapata matokeo mazuri ili kuendelea kubaki katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.




KMC FC ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake miwili mfululizo tangu kumalizika kwa mapumziko ya wiki mbili kupisha michuano ya Kimataifa, imewahakikishia mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuwa hivi sasa kila mechi imejipanga kupata matkeo amzuri.

Hakuna mechi ambayo kwetu itatushinda kupata matoke, hata kama tunacheza na Timu ya namna gani, ndio mana tunasema Pira Spana, Pira Mapato,Pira Kodi , tunachokihitaji hivi sasa ni ushindi tu na sio vinginevyo,hivyo hata mechi hii ipo ndani ya uwezo wetu.

Itakumbukwa kuwa KMC FC imewahi kupata matokeo mazuri katika michezo mitatu ya ugenini ambayo ni dhidi ya Mwadui ambapo ilipata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri, mchezo dhidi ya Gwambia ilipataushindi wa magoli matatu kwa sifuri pamoja na mchezo dhidi ya Bishara iliyotoka sare ya bao moja kwa moja

Hali ya kikosi ipo vizuri, tumeweza kufanya maandalizi ya kutosha na ni wahakikishie mechi dhidi ya Mtibwa ipo ndani ya uwezo wetu, tunauhakika wakuchukua alama tatu ,hivyo tunakwenda kifua mbele za kuchukua alama tatu ugenini.

Imeandaliwa na

Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news