Leicester City yatoshana nguvu na Manchester United 2-2

Leicester City imetoshana nguvu na Manchester United baada ya kutoka dimbani wakiwa na mfanano wa mabao 2-0.
Jamie Vardy (kushoto) wa Leicester City akishangilia na James Maddison baada ya kutupia bao la pili. (Picha na Michael Regan/Pool/Reuters). 

Mtanange huo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa katika dimba la King Power Stadium wababe hao wameonekana kucheza kwa kasi, hali ambayo imesababisha matokeo hayo yapatikane.

Ni katika mtanange huo mtamu ambapo kipindi cha kwanza wachezaji wote walikwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wamefungana bao 1-1 ambapo Marcus Rashford alianza kutupia dakika ya 23 likasawazishwa na Harvey Barnes dakika ya 31.

Aidha, kipindi cha pili kila timu ilikuwa ikipambana kusaka ushindi ambapo Manchester United kama kawaida yao walianza kupata bao la kuongoza.

Baadae Bruno Fernandes dakika ya 79 alipachika bao la pili kwa Manchester United ambalo lilisawazishwa na Jamie Vardy dakika ya 85.

Matokeo haya yanaifanya Manchester United ikiwa imecheza mechi 14 kuwa nafasi ya tatu na alama 27 huku Leicester City imecheza mechi 15 ikiwa nafasi ya pili na alama 28.

Post a Comment

0 Comments